Ni mengi yaliyosemwa juu yangu
Na ni wengi waliosema mbele yangu
Kwamba sitafika kule, nitaishia hapa hapa
Sitasogea kule, nitabaki hapa hapa
Walionicheka mdomo wamefunga
Walionibeza imebaki historia
Umeniheshimisha Daddy ooh
Ukapigana vita mbele ya adui zangu
Ushuhuda halisi wa matendo yako
Ila kwako Mungu unalo NENO
Ila kwako Mungu una matendo
Ona wanavoshangaa, hawajui Bwana umefanya
Maana wakikumbuka nyuma, huwakujua nini ulipanga
Sijawahi ona mwenye haki wako umemuacha
Wala watoto wote wa kizazi chake kuhangaika
Ukapigana vita mbele ya adui zangu
Ushuhuda halisi wa matendo yako
Ila kwako Mungu unalo NENO
Ila kwako Mungu una matendo