Africa Simama - Sauti moja ongea
Africa Simama - Sauti moja ongea
Leta Kayamba na Marimba twende sawa
Jogoo alikua Simba alipowika na akauwawa
Mwenye nyumba amenifunza kabla ya kula kunawa
Ndio kuna ndumba na ilikua kinga kwa mzawa
Wanauliza kwa nini kizazi kinapagawa
Hizi Story za Mohaa na Jesus Zinatugawa
Tunaitwa Maskini Na Nchi imejaa Kahawa
Tunaitwa Maskini na Nchi imejaa vipawa
Tukiungana tutafika mbali sio lazima tuwe na mbawa
wakumbushe rasilimali zetu ni urithi wa mzawa
Mara Moja sumu Mwarubaini kwetu dawa
Leo wanaojenga Reherb ndio wanaosambaza dawa
Tumechoka kuletewa maradhi alafu waje kutupa tiba
Wanauwa tunaowapenda alafu wahudhurie misiba
Wanatulaza njaa alafu wanauliza ka tumeshiba
Tusimame kupaza sauti kama alivyofanya Madiba
Africa Simama - Sauti moja ongea
Africa Simama - Sauti moja ongea
Walituletea Njaa na Magonjwa kuhakikisha tunawahitaji
Kwetu hakuna misaada kama hatufanyi hivi sijui ni vile
watu Weusi ni wakukaliwa tangu kale
Tulipunguziwa Ukatili Kiakili watutawale
Nje ndani wanatujua tunaishi jana Yao
ona masoko yetu yalivyojaa bidhaa zao
Bidhaa zetu wananunua kwa bei zao
Mfumo wa Elimu kila mwaka unazidi kuchuja ili
Wanaohitaji ajira kwa malipo duni wasije pungua idadi
mahasidi walipanaga kila kitu pia uvamizi wa magaidi
kila siku tuishi na taharuki
kama sio Mungiki ni Alshabab au makundi mengine ya ajabu
Tabu zetu wanazijua sababu
Rasilimali zote ni zao wajinga ndio waliwao.
Africa Simama - Sauti moja ongea
Africa Simama - Sauti moja ongea
Amka uliyelala osha uso toa matongo
Unakataa Kuitwa mtumwa na bado unaongea kimomo
Africa Sio Mama Si Baba ni wazazi wote
Wewe Na Mimi tuinuke tuimbe wote.
Africa Jungu Kuu Daima haliishiwi na ukoko
Japo wapo wanoko hawataki tuwe moko
Twatengana kwa ukabila na mengi ya kijinga
Viongozi wakija na hila twashikiana Silaha
Mida tunazozana rasilimali inaporwa
Mwafrika anajidharau ni sharti kudharauliwa
lazima tujidhamini na tudhamini vya kwetu
Tuinue viwanda vyetu tuanze kununua vya kwetu
Tuinue uchumi wetu tuelimishe vizazi vyetu
Tujiite majina yetu tujione fahari vya kwetu
bila viongozi wetu tupige hatua kivyetu
ndani ya umoja wetu ndio upo ukombozi wetu
hamna mida ya kulaumiana au kunyosheana vidole
tugange yajayo yalio pita si ndwele
Tukiendelea kufwata nyayo lini tutakua mbele
sio rahisi hapakosi vikwazo tele
Africa niisimame sasa ama ibaki chini milele
Afrika iongee ama ibaki kimya milele
Tena bila uoga tuimbe kwa sauti moja
imfikie kila muhusika manake huu ndio wakati
Africa Simama - Sauti moja ongea
Africa Simama - Sauti moja ongea