Najua ushanivumilia mambo kibao
Lakini haukuchoka ukakang'ang'ana na mie
Na sio kiangazi masika na sie tutafika (nivumilie)
Na maisha matuta kama nikianguka (ninyanyue)
Ila simaanishi nimefeli, kwangu mambo bado
Walishanikwamisha matapeli, wakaharibu mambo
Na usije wakakurubuni kwa punje za mtama, ukaniacha mie
Nitakulinda nitakutunza ka' mboni ya jicho langu,
Na sitojali mangapi wanasema wanateta,
Tunapendezana, ooh iwe kwa shida na raha
Tutaongozana, mi na wewe hata tukilala njaa
Tunapendezana, mmh wawili kama mapacha
Tutaongozana, ooh mi na wewe baby
Najua sometimes unawaza hulali
Mawazo maswali nitapata lini (nitapata lini)
Kumekuchosha uswahilini nyumba za kupanga,
Ndani joto kali (ndani joto kali),
Na kuna muda naota wamekubeba wenye mali unaishi Masaki,
Hakuna ndoto iliyoboa ile siku nakufuma napigwa risasi,
Na hakuna siku nitaumia sana kama itakupoteza nafsi (itakupoteza nafsi)
Na usije wakakurubuni kwa punje za mtama, ukaniacha mie
Nitakulinda nitakutunza ka' mboni ya jicho langu,
Na sitojali mangapi wanasema wanateta,
Tunapendezana, tunapendezana mi na wewe
Tutaongozana, wawili tu tutaongozana milele
Tunapendezana, tunapendezana mi na wewe kama mapacha
Tutaongozana, tutaongozana (aaaahh aaaaahh) tutaongozana mi na wewe, kama mapacha